Mseto wa vita na mazingaombwe ili kuunda War Legends - mchezo halisi wa kale wa kimkakati katika muda halisi, unaoangazia ulimwengu dhahania ulio na mazimwi na binadamu, majitu na mbilikimo, mapepo, mizimu, mashujaa wa ajabu na uchawi.
War Legends ni mchezo wa kipekee wa vitu kwenye simu zilizo mtandaoni, ambao ni wa kimkakati katika muda halisi kutoka michezo ya kale ya RTS kwenye PC! Unajumuisha mbinu zote za kale za michezo ya RTS kwenye simu yako. Kuza kituo chako, tafuta rasilimali kama vile dhahabu na mbao, ajiri askari, unda mitambo ya vita na uwaite mashujaa ili wavamie maadui na kupata ushindi. Amrisha na usimamie jeshi lako katika vita vya PvP, tumia aina mbalimbali za mbinu za vita, tumia uchawi, zingira kituo cha adui na ushinde ulimwengu dhahania.
Chagua upande wako katika makabiliano yasiyo na kikomo kati miungano ya Mwanga na Giza. Makundi sita ya ajabu yanakusubiri. Kila kundi lina vifaa vya kipekee vya vita! Maajabu ya kupona ya majitu, matambiko ya mizimu, visu vikali vya binadamu, hasira ya mazimwi, uvumbuzi hatari wa mapepo na teknolojia ya kipekee ya mbilikimo - yatumie kwa busara kushinda mapambano ya PVE na PVP.
Mchezo huu wa MMO RTS unaangazia mazingira mbalimbali ya mapambano ya wachezaji wengi wanaoshindana, kuanzia mapambano rahisi ya PvP hadi mapigano ya vikundi ya 2vs2 na 3vs3, vita vya FFA, uwanja, na hata mashindano yenye zawadi za ajabu. Changanya mbinu zako kwa hekima pamoja na jamii yako katika mapambano ya kushirikiana ili jamii yako ipate ushindi.
War Legends ni mchezo wa kimkakati unaochezwa bila malipo, ambao unakuruhusu uimarishe jeshi lako - vitengo, mashujaa, majengo na mabango. Vitu mbalimbali vinakupa uwezo usio na mwisho wa kubadilisha vitengo na mashujaa upendavyo. Unakuruhusu ubuni mbinu za kipekee za ushindi. Ni mchezo unaohitaji ujuzi.
★ Mchezo wa kale wa RTS umetumia mbinu zote bora kutoka kwenye aina bora za kale za PC.
★ Mchezo wa wachezaji wengi wenye mapambano ya kuvutia ya PVP, 2vs2, 3vs3 na kiushirika (kushirikiana).
★ Mapambano maalum ya PvP na marafiki zako. Hadi wachezaji 6 mtandaoni katika pambano moja.
★ Picha za kina na za kuvutia za 3D zitakushirikisha kikamilifu.
★ Makundi sita ya ajabu: mazimwi na wanadamu, majitu na mbilikimo, mapepo, na mizimu.
★ Mabango ya kivita yaliyo na nguvu kuu za uchawi.
★ Mchezo wa kimkakati wa MMO. Maelfu ya wachezaji mtandaoni kutoka ulimwenguni kote.
★ Imarisha na ubadilishe jeshi lako upendavyo.
★ Kampeni kuu ya PVE inayoongozwa na hadithi kwa kila upande, ikiwemo misheni za kujinusuru.
★ Ungana na marafiki mpambane katika vita vya kijamii.
Mchezo huu wa mtandaoni wa kimkakati unaohusu vita katika muda halisi (RTS) unakufanya uhisi shujaa kwenye makabiliano yasiyoisha kati ya mema na maovu. Amrisha, shinda, tengeneza kasri, ita mashujaa na utumie uchawi kuongoza jeshi lako lishinde. Imarisha jeshi lako na ubuni vitu vya kipekee kama vile ngao, silaha na hirizi ili upange mashujaa na vitengo jinsi unavyotaka.
War Legends ni mchezo wa mtandaoni unaohusisha wachezaji wengi. Unahitaji intaneti thabiti. Kumbuka kuwa huwezi kuucheza bila intaneti.
Ukipata tatizo lolote unapoucheza au ukiwa na maoni, tafadhali wasiliana nasi kupitia hello@spirecraft.games. Tunathamini maoni yako na tuko tayari kuboresha michezo yetu ili ifurahishe wachezaji wetu.
Ilisasishwa tarehe
18 Mei 2025
Ya ushindani ya wachezaji wengi